© Copyright Jim Goldberg/Magnum Photos 

 Mateso ni Nini?

Mateso ni tendo za kusudi ambazo husababisha maumivu makali ya kimwili au kiakili, kwalengo la kusababisha hofu au vitisho, kupata habari fulani au kukiri, kuadhibu, au kwasababu yeyote inayohusika na ubaguzi wa aina yeyote. Kunazo sheria maalum ya kimataifa yanayoangazia maswala ya mateso haswa katika mataifa ambayo yanaruhusu vitendo hivi.

Iwapo vitendo hivi vinatendwa na mtu binafsi, na serikali inashindwa kuwaadhibu au kuwapa onyo vilivyo, basi serikali inaweza kuwajibika kwa vitendo hivi na pia kuonekana kama kutojali kuzingatia sheria.

Mara nyingi mateso hutumika kama njia ya kuadhibu mtu, kupata habari au kukiri, kutisha mtu ama kama njia ya ubaguzi.

Njia ambazo hutumiwa kutesa watu kwa kawaida ni kama: kumpiga mtu, ubakaji na unyanyashaji kijinsia, kushtushwa kwa umememe,kutandaza miili, kukatazwa au kunyimwa usingizi,uzamishaji majini, kaba/kukabwa hewa, kuchomwa kwa moto, vitisho, kutengwa, udhalilishaji, kutishiwa kuuawa, na kushuhudia mateso ya wengine.

Maktaba muhimu ya kimataifa ambayo yanafafanua mateso ni Maktaba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Mateso na vitendo vingine vya kinyama au udhalilishaji au vya kuadhibisha(1984):

Kifungo cha 1 cha Maktaba dhidi ya mateso inaainasha ya kwamba:

“...Mateso ina maanisha tendo lolote ambalo linasababisha maumivu ama kuteseka, iwe kimwili au kimawazo”ambayo lina kusudi la kupata habari au kukiri, kuadhibu mtu  kwasababu  la tendo lake au la mtu mwingine au ni watuhumiwa, au kwa vitisho kumlazimisha mtu yeyote  kutokana na ubaguzi kukiri au kutenda jambo fulani, mateso yakisababishwa na au kwa niaba ya au na kibali ya mfanyikazi wa umma au mtu yeyote mwenye cheo rasmi.[...]” .

Tunaweza kutoa ushauri kibinafsi ili kuweza kutambua kanakwamba umepitia mateso. Vitendo vya kinyama, kikatili, udhalilishaji na pia kuadhibu vimepigwa marufuku na ni mambo ambayo tunaweza kusaidia nayo. 


Back to Top

Swahili

 

Website by Adept