© Copyright Jim Goldberg/Magnum Photos

Jinsi tunavyo toa usaidizi?

Unaweza kuvutiwa na:

1.  Kutafuta haki [tovuti ya kesi]

Redress hutoa ushauri wa kisheria kwa waathiriwa ambao wanatafuta njia ya kupata suluhisho kwa yale mateso waliopitia pamoja na msaada wa kupata ushahidi. Kuna njia tofauti za ufumbuzi ya maswala ya mateso kulingana na kila kesi. Haki kutokana na kesi ya mateso inaweza kuwa kwa njia ya kulipwa fidia kutokana na hasara ambayo umepata, utambuzi wa mateso rasmi  kutoka kwa mahakama,uchunguzi wa makosa ya jinai dhidi ya wahusika na baadhi mengine ya kukiri madhara waathiriwa wamepata.

REDRESS inaweza kusaidia waathiriwa kwa njia ya moja kwa moja, kwa kufanya kazi na wanasheria nchini Uingereza au mashirika mengine au wanasheria kutoka nchi ambapo mateso yalitokea.

Kwa kufuata tovuti  lifuatayo, unaweza kusoma kuhusu mifano ya kazi yetu

2.  Kuleta Mashtaka dhidi ya Watesaji

Tunaweza kujaribu kuleta mashtaka dhidi ya watu ambaye wamehusika  na vitendo vya mateso kulingana na mahala watesaji hao wanapatikana ikiwa nchini mwao ama nchi za kigeni geni. Kwa wakati mwingine jambo hili huambatanishwa na juhudi zetu ya kutafuta haki.

3. Utetezi [tovuti ya ‘Mahali ambapo tuna fanya kazi]

Tunaweza pia kuchangia ongezeko la utambulishaji la kesi lako mbele ya shirika za haki ya kibinadamu zinazopataikana kitaifa, za kikanda au kimataifa au mbele ya Umoja wa Kimataifa.

Ukiwasiliana nasi Ili uweze kupata ushauri kulingana na njia tofauti zinazoweza kutumiwa kutekeleza utetezi, nu muhimu utujulishe mahali au nchi ambapo mateso yalitendeka. Hii itatuwezesha kwa kukushauri kuhusu njia tofauti unayoweza kutumia katika hali ya utetezi.

4. Ushauri na Msaada

REDRESS hujaribu kutoa msaada kwa njia zingine tofauti, kwa mfano, sisi:

 

 5. Elimu na Ushauri

REDRESS hutoa utaalamu kwa kutazama maoni tofauti za kisheria  kwa shirika tofauti za serekali , wanasheria na mahakama za kitaifa na kimataifa.  Tunaweza pia kutoa mafunzo kuhusu njia za uhifadhi wa mateso. We can also providing training on Documenting Torture.  [Tovuti cha kurasa La Uhifadhi wa Nayraka za Mateso]  [Link to Documenting Torture page]

 Mateso ni Nini?

Mateso ni tendo za kusudi ambazo husababisha maumivu makali ya kimwili au kiakili, kwalengo la kusababisha hofu au vitisho, kupata habari fulani au kukiri, kuadhibu, au kwasababu yeyote inayohusika na ubaguzi wa aina yeyote. Kunazo sheria maalum ya kimataifa yanayoangazia maswala ya mateso haswa katika mataifa ambayo yanaruhusu vitendo hivi.

Iwapo vitendo hivi vinatendwa na mtu binafsi, na serikali inashindwa kuwaadhibu au kuwapa onyo vilivyo, basi serikali inaweza kuwajibika kwa vitendo hivi na pia kuonekana kama kutojali kuzingatia sheria.

Mara nyingi mateso hutumika kama njia ya kuadhibu mtu, kupata habari au kukiri, kutisha mtu ama kama njia ya ubaguzi.

Njia ambazo hutumiwa kutesa watu kwa kawaida ni kama: kumpiga mtu, ubakaji na unyanyashaji kijinsia, kushtushwa kwa umememe,kutandaza miili, kukatazwa au kunyimwa usingizi,uzamishaji majini, kaba/kukabwa hewa, kuchomwa kwa moto, vitisho, kutengwa, udhalilishaji, kutishiwa kuuawa, na kushuhudia mateso ya wengine.

Maktaba muhimu ya kimataifa ambayo yanafafanua mateso ni Maktaba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Mateso na vitendo vingine vya kinyama au udhalilishaji au vya kuadhibisha(1984):

Kifungo cha 1 cha Maktaba dhidi ya mateso inaainasha ya kwamba:

“...Mateso ina maanisha tendo lolote ambalo linasababisha maumivu ama kuteseka, iwe kimwili au kimawazo”ambayo lina kusudi la kupata habari au kukiri, kuadhibu mtu  kwasababu  la tendo lake au la mtu mwingine au ni watuhumiwa, au kwa vitisho kumlazimisha mtu yeyote  kutokana na ubaguzi kukiri au kutenda jambo fulani, mateso yakisababishwa na au kwa niaba ya au na kibali ya mfanyikazi wa umma au mtu yeyote mwenye cheo rasmi.[...]” .

Tunaweza kutoa ushauri kibinafsi ili kuweza kutambua kanakwamba umepitia mateso. Vitendo vya kinyama, kikatili, udhalilishaji na pia kuadhibu vimepigwa marufuku na ni mambo ambayo tunaweza kusaidia nayo. 


Back to Top

Swahili

 

 

 

 

 

Website by Adept